Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inahofia hukumu kali zinazotolewa Bahrain

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inahofia hukumu kali zinazotolewa Bahrain

 

Kesi zilizoendeshwa nchini Bahrain na kushuhudiwa wanaharakati wa kisiasa wakihukumiwa kifungo cha maisha zimeelezewa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kama ni hatua za mateso ya kisiasa. Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema haki za wanaharakati wa kisiasa 21 hazikuheshimiwa wakati wa kesi hizo.

Kamishina mkuu amesema kesi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakidai demokrasia kwenye mahakama ya usalama wa taifa nchini Bahrain ni lazima zisitishwe na washitakiwa wapewe fursa ya kuwa na kesi huru na zinazozingatia misingi ya haki.

Watu takribani 100 wamefungwa jela na mahakama hiyo huku wengine 1000 wako mahabusu wakisubiri kesi . Ravina Shamdasani ni kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Geneva.

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASANI)

Kamishina mkuu amesema anatuma barua kwa mfalme wa Bahrain kuelezea hofu yake dhidi ya wanavyotendewa raia na watetezi wa haki za binadamu nchini humo.