Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 600,000 wamekimbia tangu kuzuka machafuko Libya:OCHA

Zaidi ya watu 600,000 wamekimbia tangu kuzuka machafuko Libya:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema takribani watu 530,000 wameshapokea msaada wa chakula ndani ya Libya, ingawa kuna taarifa za mapigano makali yanayoendelea katika sehemu za Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa OCHA mahitaji mapya ya kibinadamu yamebainika , yakiwemo matatizo makubwa ya kiusalama kutokana na masalia ya silaha za vita. Tangu kuzuka kwa machafuko watu zaidi ya 650,000 wameondoka nchini Libya na kuanzia wiki jana mapigano yameshika kasi Kaskazini Magharibi hasa maeneo ya Zlitan, Khums, Brega, Misrata, Zawyiah na baadhi ya maeneo ya milimani ya Nafusa.

OCHA inasema ingawa msaada unawafikia waathirika, vikwazo na hasa wa kisalama vinaendelea kutia dosari operesheni za misaada na kutathimini hali halisi ya mahitaji ya kibinadamu.