Mamia ya watoto wanaokimbia Libya na wako katika hatari ya kufanyiwa dhuluma:IOM

24 Juni 2011

Mamia ya watoto ambao wako peke yao na watoto wahamiaji waliotenganishwa na wazazi wao kutokana na machafuko yanayoendelea Libya wako katika hatari ya kutendewa ukatili, kunyonywa na kufanyiwa ghasia kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Watoto wao wanajumuisha wasichana ambao waliingizwa kinyemela Libya ili kufanya kazi na kusoma kutoka nchi za Afrika ya magharibi na wakajikuta wakiishia kwenye biashara ya ukahaba.

IOM inasema watoto zaidi ya 150 wasio na wazazi wao na wengine wamewekwa katika ulinzi maalumu ingawa idadi ya wanaohitaji kulindwa inaweza kuwa kubwa. Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM anasema watoto hao wako katika hali ya hatari na wanatafuta usalama kwenye makambi ya wakimbizi wa ndani kwenye mpaka wa Libya na Tunisia.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

IOM inasema inashirikiana na mashirika mengine ikiwemo UNICEF ili kujaribu kuwaunganisha tena watoto hao na familia zao.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter