Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 20,000 wa Kisomali wawasili Kenya katika muda wa wiki mbili:UNHCR

Wakimbizi 20,000 wa Kisomali wawasili Kenya katika muda wa wiki mbili:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limetiwa hofu na ongezeko la ghafla la wakimbizi wanaowasili Kenya wakitiokea Somalia. Katika muda wa wiki mbili zilizopita kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko Kaskazini mwa Kenya imepokea wakimbizi wa Kisomali zaidi ya 20,000 kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR Melisa Fleming.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

UNHCR inasema wengi wa wakimbizi hao ni wakulima na wafugaji kutoka lower Juba na mji wa Dhobley. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu kambi ya Dadaab imepokea wakimbizi wapya 55,000 na idadi inaongezeka kwa watu 1300 wanawasili kila siku. UNHCR inashirikiana na serikali ya Kenya na mashirika mengine ya misaada kukabiliana na hali hiyo.