Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imetolea wito serikali ya Msumbiji kutowarejesha kwa nguvu waomba hifadhi

UNHCR imetolea wito serikali ya Msumbiji kutowarejesha kwa nguvu waomba hifadhi

Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema waomba hifadhi 93 wamerejeshwa kwa nguvu kutoka Msumbiji hadi Tanzania Jumanne asubuhi wiki hii.

Waomba hifadhi hao ni pamoja na Wasomali 59 na Waethiopia 34 ambao waliwasili hivi karibuni kwa boti karibu na jimbo la Mocimboa da Praia Kaskazini mwa Msumbiji. Watu hao wengi ni wavulana, lakini pia  mwanamke mmoja, watoto wane na wazee watatu, na wengi wana matatizo ya kiafya kwa sababu ya safari ndefu. Afisa wa UNHCH aliyekutana na watu hao jimboni Micimboa da Praia hakujua kama wanarejeshwa kwa nguvu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)