Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya Haki za binadamu kutuma ujumbe Yemeni

Ofisi ya Haki za binadamu kutuma ujumbe Yemeni

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inajiandaa kupeleka ujumbe nchini Yemen Jumatatu ijayo Juni 27 ili kutathimini hali ya haki za binadamu kufuatia matukio ya machafuko ya karibuni.

Ujumbe huo wa wataalamu wa haki za binadamu utakuwa Yemen kwa siku 10 hadi Julai 6 kukusanya taarifa kuhusu hali ya haki za binadam, kwa kukutana na maafisa wa serikali, watetezi wa haki za binadamu, wahanga wa kiukaji wa haki za binadamu, viongozi wa kisiasa wa upinzani, jumiya za kijamii, pia viongozi wa dini na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Ujumbe huo pia utajitahidi kukutana na wakimbizi wa ndani na una mpango wa kuzuru vituo vya afya na mahabusu katika miji mbalimbali. Wakati wa kufanya tathimini wataalamu hao watatoa ripoti ya awali ambayo itajumisha mapendekezo kwa wadau wote ikiwemo pande husika nchini yemen na jumuiya ya kimataifa.

Ripoti hiyo itawekwa wazi na kuwasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu kwenye kikao chake cha Septemba mwaka huu.Tathimini hiyo inafanyika kwa ushirikiano na wizara ya mambo ya nje ya Yemen.