Baada ya kisa mkasa wajane wakabiliwa na adha chungu nzima

23 Juni 2011

Kina mama wajane kote duniani wanakabiliwa na matatizo mengi, kuanzia ngazi ya familia, jamii , kitaifa na hata kimataifa. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kuna wajane zaidi ya milioni 245 na zaidi ya nusu wanakabiliwa na kuishi kwenye umasikini mkubwa hasa katika nchi zinazoendelea.

Sababu za wajane hawa ambao wamepoteza wame zao na kusalia na mzigo wa familia kuendelea kunyanyasika ni mila na desturi, lakini pia serikali nyingi hazina sera, sheria wala mipango ya kuwalinda na kuwasaidia wajane.

Sasa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka nchi zote kuhakikisha wajane wanalindwa, na haki zao zinazingatiwa iwe katika mirathi, umilikaji ardhi,ajira na hata haki zao za binadamu. Sikiliza masahibu yanayomkabili mama huyu mjane kutoka Kenya.

(MAELEZO YA MARRY MURAA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud