Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hatua ya kuruhusu ujenzi wa majego Gaza

UM wakaribisha hatua ya kuruhusu ujenzi wa majego Gaza

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati amekaribisha kwa moyo mkunjufu hatua ya Israel ambayo imetangaza kuruhusu umoja huo wa mataifa kuendesha ujenzi wa maeneo kadhaa kwenye ukingo wa Gaza.

Robert Serry ambaye anaratibu shughuli za umoja wa mataifa kwenye eneo hilo amesema kuwa uamuzi huo uliotangazwa na Israel ni hatua inayotia matumaini.Israel ilitangaza kuwa iko tayari kuliruhusu shirika la Umoja wa Mataifa linaloendesha shughuli za misaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA kuendesha ujenzi wa majengo kwenye eneo hilo la Gaza. Uamuzi huo ni matunda ya majadiliano baina ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak