Zoezi la kuwarejesha kwenye jamii ya kawaida askari watoto Chad linahitaji msaada zaidi:UM

Zoezi la kuwarejesha kwenye jamii ya kawaida askari watoto Chad linahitaji msaada zaidi:UM

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali za watoto waliko kwenye maeneo yaliyokumbwa na mizozo ya silaha amesema kuwa Chad itahitaji msaada zaidi wakati wa utekelezaji wa mpango ambao umelenga kuwaunganisha askari waototo katika jamii ya kawaida.

Radhika Coomaraswamy hivi karibuni alitembelea Chad ambako alijionea hali mbalimbali zinavyowaandama askari hao watoto na changamoto iliyo mbele wakati wa utekelezwaji wa zoezi hilo.Pia alishuhudia mpango mkakati ambao umetiwa saini na pande zote zinazohasimiana wenye shabaya ya kuanza kuwarejesha askari watoto kwenye jamii ya kawaida.Wakati wa utekelezwaji wa zoezi hilo Umoja wa Mataifa umesema kuwa utafuatilia kwa karibu na wakati huo itawasajili watoto hao ili baadaye kujua mwenendo wao huko waliko.