Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM aitaka Sudan Kusini kutia sahihi mikataba muhimu ya haki za binadamu

Afisa wa UM aitaka Sudan Kusini kutia sahihi mikataba muhimu ya haki za binadamu

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa anasema kuwa eneo la Sudan Kusini ambalo hivi karibuni litakuwa taifa huru linastahili kuhakikisha kuwa wananchi wake wanafurahia uhuru mara litakapotangazwa huru. Akiwahutubia wanafunzi , wanadiplomasia na vyombo vya habari waliokusanyika kwenye chuo cha Juba Kyung-wha Kang, naibu kamishina wa haki za binadamu amesema kuwa Sudan Kusini ni lazima ionyeshe kujitolea katika kuwa taifa lenye demokrasia ambapo watu wana haki sawa.

Bi Kang ameishauri serikali ya Sudan kutia sahihi mikataba yote inayohusiana na haki za binadamu na kuweka sheria zitakazowalinda wananchi na kuboresha haki za binadamu.