Ban akaribisha mabadiliko ya katiba nchini Morocco

Ban akaribisha mabadiliko ya katiba nchini Morocco

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha mapendekezo yaliyo kwenye mpango wa kuifanyia mabadiliko katiba ambayo serikali ya Morocco itayatoa kwa wananchi wakati wa kura ya maoni mwezi July. Kupitia kwa taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban pia amewapongeza wananchi na serikali ya Morocco kwa njia ambayo wamekuwa wakiendesha shughuli za mabadiliko ya kisiasa.

Ban pia anasema kuwa anaamini kuwa mpango huo wa mabadiliko utaheshimu matakwa ya wananchi wa Morocco. Mabadiliko ya katiba nchini Morocco yanajiri wakati nchini nyingi kaskazini mwa Afrika na mashariki ya kati zinapokumbwa na mizozo.