Skip to main content

Ban amezitaka jamii kuwawezesha wajane ili wawe na jukumu la maana kwenye jamii

Ban amezitaka jamii kuwawezesha wajane ili wawe na jukumu la maana kwenye jamii

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amezitaka jamii kupunguza adha wanazokabiliana nazo wajane baada ya kufiwa na waume zao , kwa kuheshimu haki zao, katika masuala ya mirathi, umuliki wa ardhi, ajira na mipango mingine ya kuwawezesha kuishi.

Ban amesisitiza kwamba wajane wote lazima walindwe kwa kuzingatia mkataba unaotaka mifumo yote ya ubaguzi dhidi ya wanawake ikomeshwe, na mikataba mingine ya haki za binadamu. Ban ameyasema hayo katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha kwa mara ya kwanza siku ya kimataifa ya wajane ambayo kuanzia leo itakuwa ikifanyika kila mwaka tarehe 23 June. Mamama…………ni mjane kutoka nchini Kenya

(SAUTI YA MJANE)

Ban amesema kifo hakiepukiki lakini jamii zinaweza kupunguza machungu ya kufiwa kwa wajane kwa kuinua hadhi yao wakati wanapohitaji. Amesema hili litachangia kuchagiza ushiriki sawia wa wanawake wote katika jamii na kuendeleza taifa lao.Je watu mbalimbali wana maoni gani kuhsu siku hii?

(MAONI YA WAJANE)

Siku hii ilipitishwa na baraza kuu la Umoja wa mataifa mwaka jana katika juhudi za kuelezea ukiukwaji wa haki za wanawake wajane kwa nia ya kuhakikisha wanalindwa na kuwezeshwa kitaifa na kimataifa. Inakadiriwa kwamba kuna wajane takiribani milioni 245 duniani na zaidi ya milioni 115 wanaishi kwenye umasikini uliokithiri hasa katika nchi zilizoathirika na vita.