Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku ya utumishi wa umma duniani Ban amechagiza kudumisha utawala bora

Katika siku ya utumishi wa umma duniani Ban amechagiza kudumisha utawala bora

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amewachagiza watumishi wa umma kote duniani kupigia upatu masuala ya utawala bora, uwajibikaji, kuheshimu maingiliano ya mila, usawa wa kijinsia na kutumia teknolojia kwa kutumia busara na uongozi kujenga maisha bora kwa wote.

Leo ambayo ni siku ya utumishi wa umma duniani Ban amesema tunawaenzi wale waliokubali kubeba majukumu ya huduma kwa umma na waliochangia kiutendaji na kiubunifu kwenye taasisi za umma. Kwa mara ya kwanza siku hii inaadhimishwa bararani Afrika na ni jijini Dar es salaam Tanzania. Katika ujumbe maalumu wa Umoja wa mataifa Visero Akwaro akizungumza kwa niaba ya  afisa moja wa idara ya uongozi na utawala ya Umoja wa mataifa DESA amesema uongozi bora ni chachu ya maendeleo katika jamii

(SAUTI YA VISERO AKWARO)

Ameongeza kuwa kwa kutekeleza majukumu yao na kuzingatia matakwa ya ma serikali nyingi duniani zitaweza kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015.