Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kusherehekea kutokomezwa kimataifa kwa ugonjwa wa Sokota

FAO kusherehekea kutokomezwa kimataifa kwa ugonjwa wa Sokota

Mkurgenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Jacques Diouf atazindua hafla maalumu kusherehekea dunia kuwa huru na maradhi yanayokatili maisha ya ng’ombe ya Sotoka.

Sotoka ni moja wa magonjwa hatari ya mifugo ambayo yameisumbua dunia kwa muda mrefu na yamekuwa pia tishio kwa maisha ya binadamu na usalama wa chakula. Kutokomezwa kwa ugonjwa huo kulikoongozwa na FAO na washirika wake kunafanya virusi vya sotoka kuwa ndio vya kwanza vya mifugo kutokomezwa kabisa na vya pili duniani kuumalizwa baada ya ndui iliyowaathiri binadamu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)