Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM apongeza mkataba mpya wa ILO unaowalinda wafanyakazi wa majumbani

Afisa wa UM apongeza mkataba mpya wa ILO unaowalinda wafanyakazi wa majumbani

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ambaye anahusika na usimamizi wa kamati inay oangazia haki za wahamiaji amekaribisha hatua iliyofikiwa na shirika la kazi ulimwenguni ILO ambayo imepitisha rasmi sheria zinazohusu wafanyakazi wa majumbani.

Afisa huyo amesema kuwa mamilioni ya wafanyakazi wa majumbani wapo hatarini wakikumbana na vitendo vya unyanyaswaji na kutumikishwa kwa nguvu hivyo kupitishwa kwa  mwongozo huo mpya kutaleta faraja kwao.

Mtaalamu huyo Abdelhamid El Jamri,amesema wanawake na watoto wa kike ndiyo wanatumbukia zaidi kwenye kazi hizo ambazo wakati mwingine hazizingati ustawi wao.Ametaka mataifa kuharakisha uridhia wa sheria hiyo ili hatimaye ipate baraza na kuanza kutumika duniani kote.