Hifadhi ya India yaondoka kwenye mkondo wa hatari: UNESCO

22 Juni 2011

Hifadhi moja iliyoko nchini India ambayo awali iliorodheshwa kuwa miongoni mwa hifadhi za uridhi wa dunia zilizopo kwenye hatari sasa imeondolewa.Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limesema leo hifadhi hiyo inayojulikana kama Manas sasa imeondolewa kwenye orodha hiyo kufuatia maendeleo makubwa yaliyopigwa katika miaka ya hivi karibi.

Hifadhi hiyo ambayo inautajiri mkubwa wa viumbe ilikuwa hatarini kutoweka kutokana na machafuko yaliyozuka kwenye eneo hilo ambayo yalizuka ikiwa miaka saba tu tangu UNESCO kuitaja kuwa ni miongoni mwa urithi wa dunia.Ikielezea kuimarika kwa uhafadhi wa sehemu hizo, UNESCO imesema kuwa juhudi zilizofanywa zimeanza kuleta matunda na kuondosha kabisa kiticho kilichokuwa kikiliandama eneo hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter