Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la UM laomba misaada zaidi kwa wakimbizi wa kipalestina

Shirika la UM laomba misaada zaidi kwa wakimbizi wa kipalestina

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililotwikwa jukumu la kuwasaidia mamilioni ya wakimbizi wa kipalestina amesema kuwa shirika hilo lilikumbwa na uhaba wa dola milioni 63 mwaka huu na kuwaomba wahisani kuongeza misaada yao.

Mkurugenzi wa shirika la UNRWA amesema kuwa ufadhili kutoka kwa nchi za kiarabu uliongezeka kwa asilimia tatu mwaka uliopita. Pia amesema kuwa mpango wa amani uliokwama kati ya utawala wa palestina na Israel unaongeza hatari ya kuwepo ukosefu wa utulivu katika eneo hilo. Grandi ametoa wito kwa pande husika kuchukua hatua zifaazo kumaliza mzozo uliopo , kuundwa kwa taifa la Palestina na kupata suluhu la kudumu kwa tatizo la wakimbizi.