Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD yaonya upunguzaji misaada kwa wakulima wa vijijini

IFAD yaonya upunguzaji misaada kwa wakulima wa vijijini

Umoja wa Mataifa umeonya hatua zinazochukuliwa na nchi zinazoendelea za kupunguza misaada kwa nchi maskini ikisema kuwa hali hiyo inaweza kuleta taswira mbaya hapo baadaye. Kulingana na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na mapambano ya umaskini katika maeneo ya vijijini, hatua za kupunguza misaada ya uzalishaji chakula kwa wakulima wadogo wadogo kunaweza kuleta athari mbaya na kuzaa kitisho cha njaa.

Shirika hilo limesisitiza kuwa uwezo wa wakulima hao ambao wengi wao ni maskini kuendeleza kilimo ni mdogo na hivyo kuendelea kuwapunguzia misaada kunaweza kuwafanya washindwe kabisa hata kumudu kilimo cha kujikimu wao wenyewe.

Rais wa shirika hilo IFAD Kanayo Nwanze amesema kuwa hali ya kukosekana kwa mahitaji muhimu ikiwemo chakula ilijidhihiri katika miaka ya hivi karibuni wakati wananchi walipoamua kuingua mitaani za kuzusha ghasia hivyo ametaja jambo hilo lisijirudie tena