IOM inaendelea kuwahamisha Waethiopia waliokwama Yemen

22 Juni 2011

Zaidi ya wahamiaji 1900 kutoka Ethiopia ambao wamekwama karibu na mpaka wa Yemen na Saudi Arabia wasio na njia ya kurudi nyumbani huenda wakasaidiwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wakati linarejesha shughuli zake nchini humo.

Hii ni baada ya kundi la kwanza la Waethiopia 275 wakiwemo watoto 115 na wanawake 34 kusafirishwa kutoka eneo la Haradh hadi Hodeida nchini Yemen na baadaye kusafirishwa kwa njia ya ndege hadi mjini Addis Ababa nchini Ethiopia jana Jumatatu.

Baada ya kuwasilishwa wahamiaji hao walipelekewa kwenye kituo cha IOM ambapo walipewa makao na usaidizi mwingine. Watoto wasio na wakubwa wao watakabidhiwa shirika la UNICEF na washirika wake hii leo. Afisa wa IOM Jumbe Omari Jumbe amezungumza na Alice Kariuki na kufafanua kuhusu operesheni hiyo.

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter