Jinsi wanavyotendewa raia wa Kordofan Kusini Sudan haistahiki:OCHA

Jinsi wanavyotendewa raia wa Kordofan Kusini Sudan haistahiki:OCHA

Jinsi wanavyotendewa raia wa Kordofan Kusini nchini Sudan ikiwa ni pamoja na ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu, na kuwalenga watu wa makabila fulani inasikitisha na haikubaliki amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA bi Valaries amos.

Amesema zaidi ya watu 70,000 wametawanywa na machafuko yanayoendelea katika jimbo hilo, wengine wengi wamekimbia nyumba zao na hali yao haijulikani hawa wanajumuisha wale ambao wameondoka eneo la usalama kwenye ofisi za mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan UNMIS kwenda mji wa Kadugli.

Bi Amos ameonya kwamba hali ya usalama kwa ujumla inazidi kuzorota nchini Sudan katika kiwango cha kutisha ambacho kitakuwa na athari kubwa kwa masuala ya kibinadamu.

Ametaka matatizo ya kiusalama kumalizwa na kuondoa vikwazo vya watu kutoka sehemu moja kwenda nyingi ambavyo vinaendelea kuathiri tathimini ya hali halisi, kuwafikishia msaada wanaohitaji haraka na kuingiza msaada zaidi. Pia ametaka vitisho dhidi ya wafanyakazi wa misaada na walinda amani wa Umoja wa Mataifa visitishwe mara moja.