WFP yawapongeza rais wa zamani wa Ghana na Brazil kwa kushinda tuzo ya dunia ya chakula

22 Juni 2011

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran amewapongeza marais wa zamani John Kufor wa Ghana na Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil kwa kushinda tuzo ya hadhi ya juu ya chakula duniani, iitwayo World Food Prize.

John Kufor amekuwa akiuunga mkono WFP kwa miaka mingi na kushinda tuzo hiyo kunadhihirisha umuhimu wa kazi yake duniani kote akiwa kama balozi mwema wa WFP dhidi ya njaa tangu 2009 na nyumbani kwake Ghana ambako katikamihula miwili ya utawala wake aliimarisha salama wa chakula na kupunguza umasikini kupitia sekta za umma na binafsi. Naye Lula ameelezwa kutoa mchango mkubwa kitaifa na kimataifa.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter