Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon kuteuliwa tena kuongoza chombo hicho cha kimataifa kwa muhula wa pili, baraza kuu la Umoja wa Mataifa (GA) nalo leo limechagua Rais wake mpya.
Wajumbe 192 wanachama wa Umoja wa Mataifa mchana wa leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York wamemuidhinisha balozi Nassir Abdelazizi Al-Nasser wa Qatar kuwa Rais wa kikao cha 66 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Al-Nasser ambaye anazungumza Kiarabu na Kingereza ni mwanadiplomasia wa muda mrefu, na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali ya Qatar. Al-Nasser anachukua nafasi ya Joseph Deiss Rais wa sasa takayemaliza muda wake mwisho wa Agosti na muhula mpya kuanza Septemba kinapoaanza kikao kingine cha baraza kuu. Rais wa baraza kuu huchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja.