FAO na ILO waelezea athari za dawa za kuulia wadudu kwa watoto walioajiriwa katika kilimo

22 Juni 2011

 

Jopo la pamoja la shirika la kazi duniani ILO na shirika la chakula na kilimo la moja wa Mataifa FAO limeelezea athari za dawa za kuulia wadudu kwa watoto walioajiriwa katika sekta ya kilimo.

Taarifa hiyo imetolewa kwenye mkutano mkutano maalumu mjini Geneva leo unaoajadili athari za dawa za kuulia wadudu zinazotumika katika sekta ya kilimo na makundi yaliyo hatarini hasa kwa wanawake na watoto wanaofanya kazi mashambani na juhudi za kupunguza ajira kwa watoto.

FAO na ILO wanasema dawa za kuulia wadudu ni miongoni mwa hatari kubwa wanayokumbna nayo asilimia 59 au  watoto milioni 60 walioajiriwa na kufanya kazi katika sekta ya kilimo. FAO na ILO wamesisitiza kwamba ushirikiano zaidi unahitajika miongoni mwa wadau muhimu zikiwemo serikali, watunga sera, wasajili wa dawa za kuulia wadudu, wakulima, washirika wa kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali zikiwemo sekta binafsi kama viwanda na makampuni ya biashara ili kutatua tatizo hilo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter