UM umezindua kampeni ya miaka mitano kuboresha afya na usafi kwa wote ifikapo 2015

22 Juni 2011

Mpango wa miaka mitano kuhakikisha watu wote duniani wanapata fursa ya kuwa na vyoo bora vinavyozingatia usafi umezinduliwa na Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa unasema watu bilioni 2.6 wengi wakiwa katika nchi zinazoendelea hawana vyoo maalumu vinavyozingatia maadaili ya usafi. Ukosefu wa vyoo mara nyingi husababisha madhara kama ya kuhara ambayo huchangia vifo takribani 3000 vya watoto kwa siku duniani kote. Therese Dooley mtaalamu wa afya na usafi kwenye shirika la Umoja wa mataifa la kuhdumia watoto UNICEF anafafanua kuhus mpango huo wa usafi kwa wote.

(SAUTI YA THERESE DOOLEY)

Mpango huo wa miaka mitano wa usafi endelea ulianzishwa na baraza kuu kwenye azimio lililopitishwa Desemba mwaka jana ambalo linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongeza mara mbili juhudi zao kuziba mapengo ya usafi ambalo ni moja ya malengo manane ya maendeleo ya milenia yanayopaswa kufikiwa hapo 2015

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter