Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu la UM limemteua Ban Ki-moon kuongoza UM kwa miaka mingine 5

Baraza kuu la UM limemteua Ban Ki-moon kuongoza UM kwa miaka mingine 5

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameteuliwa kuongoza chombo hiki cha kimataifa kama Katibu Mkuu kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

Ban amepata heshima hiyo baada ya wajumbe 192 wa Umoja wa Mataifa kupiga kura kwenye baraza kuu leo Jumanne Juni 21. Ban ameshukuru baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa kumuamini na kumpa tena heshima hiyo ambayo amesema daiama atailinda na kutumia wajumbe wote, kwa kila hali.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban aliuungwa mkono pia bila kupingwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Hakuna mgombea mwingine aliyejitokeza kuchuana na Ban katika kuwania wadhifa huo.

Ban aliyechaguliwa mwaka 2007 kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatoka Jamhuri ya Korea na ataanza muhula mpya wa uongozi Januari mosi mwaka 2012.