MKURABITA yaitwalia Tanzania tuzo ya UM ya utumishi wa umma

21 Juni 2011

Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA umeisaidia Tanzania kujinyakulia tuzo ya utumishi wa umma Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Umoja wa Mataifa hasa kwa kuangalia ubunifu wa kuweza kuharakisha huduma nzuri kwa umma.

Baada ya kushika nafasi ya pili mwaka jana mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika. Tuzo hiyo imetolewa sambamba na kongamano la kimataifa la utumishi wa umma linalofanyika jijini Dar es salaam Tanzania kuanzia Juni 20 na litakamilika june 23.

Wawakilishi takriban 300 kutoka nchi 80 wanashiriki kongamano hilo. Mwandishi wa Umoja wa Mataifa Stella Vuzo anafuatilia kongamano hilo na amezungumza na mkurugenzi mtendaji MKURABITA

(MAHOJIANO NA RUSIBAMAYILA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter