Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zaomba kutowarejesha nyumbani wananchi wa Haiti

Serikali zaomba kutowarejesha nyumbani wananchi wa Haiti

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa serikali kusimamisha kurejea nyumbani kwa hiyari kwa sababu za kibinadamu wananchi wa Haiti kufuatia hali mbaya iliyo bado nchini humo.

Miezi 18 baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti bado watu 680 hawajarudi makwao na kwa sasa wanaishi kwenye zaidi ya kambi 1000 kwenye mji mkuu Port-au-Prince na maeneo mengine yaliyoathirika na tetemeko la ardhi.

Hata baada ya kundaa uchaguzi mkuu na ujenzi unaondelea hivi sasa taifa la Haiti haliwezi kuwahakikishia usalama na huduma zingine wanaorejea nyumbani hasa watoto , walio na ulemavu , walio na matatizo ya kiafya pamoja na waathiriwa wa dhuluma za kingono.