Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yapata tuzo kwenye kongamano la UM na Afrika kuhusu utumishi wa umma

Tanzania yapata tuzo kwenye kongamano la UM na Afrika kuhusu utumishi wa umma

Kongamano la kimataifa la Umoja wa Mataifa na Afrika linalohusu utumishi wa umma linaendelea jijini Dar es Salaam ambako wajumbe zaidi ya 300 kutoka mataifa 80 wanajadili mbinu mbalimbali za kuboresha utumishi wa umma.

Kongamano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na nchini Tanzania linajadili kwa kina ni kwa kiasi gani utumishi wa umma unavyoweza kuharakisha kuleta maendeleo kwa wananchi.

Utumishi wa umma unachukua nafasi kubwa kwenye harakati za ustawi wa jamii. Afrika inatajwa kwamba utumushi wa umma unatoa sehemu kubwa ya ajira kwa wananchi wake na sasa inafikia zaidi ya asilimia 70. Kongamano hilo linaambatana pia na shindalo la mikakati ya kuboresha sekta ya umma barani Afrika ambapo mwaka huu Tanzania imepata tuzo.

Mpango ulioiwezesha tanzania kushinda unaitwa MKURABITA. Stephane Rusibamaila mkurugenzi muendeshaji wa MKURABITA anafafanua.

(SAUTI YA STEPHENE RUSIBAMAILA)