Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nzige wavamia Madagascar ,hatua za haraka zahitajika :FAO

Nzige wavamia Madagascar ,hatua za haraka zahitajika :FAO

 

Shirika la kilimo za mazao duniani FAO linaonya kuwa kuongezeka kwa idadi ya nzige katika eneo la kusini magharibi mwa Madagascar huenda likageuka na kuwa janga na kuhatarisha maisha ya watu milioni 13 iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kukabilina na wadudu hao waharibifu. 

Makadirio ya hivi majuzi yanaonyesha kuwa kwa sasa maeneo waliko wadudu hao yanahitaji kunyunyuziwa dawa kati ya Novemba mwaka huu na Mei mwaka 2012 kwa gharama ya dola milioni 7.6.  Afisa anayehusika na masuala ya nzige kwenye shirika la FAO Annie Monard anasema kuwa idadi ya nzige lazime ipunguzwe kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa kwenye kisiwa hicho.