Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mexico yahitaji hatua mpya kukabialina na umaskini wa chakula: De Schutter

Mexico yahitaji hatua mpya kukabialina na umaskini wa chakula: De Schutter

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya haki ya kuwa na chakula Olivier De Schutter anasema kuwa hata kama watu saba kati ya watu kumi wana uzito kupita kiasi nchini Mexico hali inayoigharimu nchi hiyi asilimo 0.5 ya pato la kitaifa bado sera za kibiashara na kilimo haziungi mkono kupatikana kwa chakula chenye afya.

Schutter amesema kuwa kujumuishwa  kwa haki ya kuwa na chakula kwenye katiba ya nchi hiyo itakuwa ni hatua kubwa akiongeza kuwa litakalofuata ni kuhakikisha kuwa kuna haki ya kuwa na chakula na kuangamiza umaskini wa chakula. Mjumbe huyo alikuwa akiongea baada ya kumaliza ziara aliyofanya nchini Mexico kati ya tarehe 13 na 20 mwezi huu kwa mwaliko wa serikali.