UM watoa wito kukabili magonjwa yasiyo ya kuambukiza

21 Juni 2011

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ametoa mwito kwa serikali,mashirika ya kiraia pamoja na watu binafsi kujitokeza kwenye mapambano ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na matumizi ya tumbaku, uchafuzi wa mazingira, vyakula na hali ya kukosa mazoezi.

Akizungumza kwenye kongamano moja ambalo linajadilia matatizo hayo, Migiro amesema kuwa Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake utajitumbukiza kwenye kampeni maalumu itayohusisha ufanyaji mazoezi na kuhamasisha ya hali ya chini ya pombe.

Migiro ambaye alikuwa akuzungumza kwenye kongamano la wataalamu wanaojiandaa na mkutano mkubwa utakaofanyika mwezi Septemba amesema jambo linalopaswa kuzingatiwa sasa ni kuwa na uamuzi wa mtu binafsi kuanza kubadili tabia.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kukabili magonjwa hayo. Hata hivyo ameongeza kusema kuwa serikali pamoja na mashirika binafsi bado yanapaswa kuchukua hatua kubwa kukabiliana na matatizo hayo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter