Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

GA inapiga kura kumchagua Katibu Mkuu mpya wa UM

GA inapiga kura kumchagua Katibu Mkuu mpya wa UM

Wajumbe 192 wanachama wa Umoja wa Mataifa watapiga kura baadaye hii leo kuchagua Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa .

Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-moon anaungwa mkono bila kupingwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na ameshasema bayana anapenda kuendelea kuongoza Umoja wa Mataifa kwa muhula wa pili wa miaka mingine mitano. Hadi sasa hakuna mgombea mwingine aliyejitokeza wazi kupingana naye.

Jean-Victor Nkolo, ni msemaji wa Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na anasema wanaopenda kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa wanahitaji kuwa na uhakika wa kuungwa mkono duniani kote

(SAUTI YA VICTOR NKOLO)

Ban Ki-moon anatoka Jamhuri ya Korea na ni Katibu Mkuu wa nane wa Umoja wa Mataifa. Wakati alipochaguliwa mara ya kwanza Ban alikuwa waziri wa mambo ya nje na biashara wa Korea. Muhula mpya unaanza Januari mosi 2012.