Mfuumo wa elimu Sudan Kusini unahitaji msaada:UNESCO

21 Juni 2011

Uhuru rasmi wa Sudan Kusini ambao hauepukiki unaleta changamoto kubwa ya kuboresha miongoni mwa mifumo mibaya zaidi ya elimu duniani umesema Umoja wa Mataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchuka hatua za haraka za kutatua na kusaidia kuanzisha mfumo wa kitaifa wa elimu Sudan Kusini.

Sudan Kusini itakuwa taifa huru Julai 9 mwaka huu na kujitenga rasmi na Kaskazini.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNESCo Irina Bokova ni vigumu kuelezea ukubwa wa changamoto, lakini uhuru wa taifa hilo unaambatana na fursa ya kujenga mfumo bora wa elimu na watu wa Sudan Kusini hawawezi kumudu kuuipoteza fursa hiyo wala jumiya ya kimataifa.

Sera iliyozinduliwa leo mjini Juba makao makuu ya Sudan Kusini inasema Sudan Kusini ina moja ya viwango vibaya kabisa vya elimu duniani, ambapo zaidi ya watoto milioni moja wanaopaswa kuwa katika elimu ya msingi hawasomi ikiwa ni karibu nusu ya watoto wote wanaopaswa kusoma.

Taifa hilo jipya ndilo lenye kiwango kidogo kabisa duniani cha wanafunzi wanaoingia sekondari. Wasichana chini ya 400 ndio wanaomaliza elimu ya sekondari na asilimia 8 pekee ya wanawake ndio wanaojua kusoma na kuandika.

Kera hiyo imetayarishwa na kitengo cha UNESCO cha elimu kwa wote (EFA), timu ya kimataifa ya kufuatilia masuala ya elimu na kundi la wataalamu huru.

Sera imeitaka serikali ya Sudan Kusini kuongeza juhudi zake binafsi katika kuboresha mfumo wa fedha, kukabiliana na kutokuwepo sawa baina ya majimbo na makundi ya watu na hatua za kuziba mapengo katika masuala ya kijinsia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter