Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angelina Jolie na mkuu wa UNCHR wakutana na wakimbizi Lampedusa

Angelina Jolie na mkuu wa UNCHR wakutana na wakimbizi Lampedusa

 

Jana Jumapili mcheza filamu nyota wa Hollywood ambaye pia ni balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Bi Angelina Jolie aliungana na mkuu wa shirika la wakimbizi kuzuru Lampedusa ambako walikutana na baadhi ya maelfu ya watu waliovuka bahari ya Mediteraniani na kuingia kwenye kisiwa hicho cha Italia wakikimbia machafuko Afrika Kaskazini.

Zaidi ya watu 40,000 wakiwemo wakimbizi na waomba hifadhi wamewasili kwa njia ya boti kisiwani Lampedusa tangu mwanzoni mwa mwaka huu kwa mujibu wa kamishina mkuu wa UNHCR. Watu hao wanajumuisha wahamiaji wa kiuchumi kutoka Tunisia, pamoja na wanaotafuta hifadhi, wakimbizi kutoka nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na Libya, ambako mapigano baina ya serikali na waasi yanaendelea. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)