Kongamano la UM na Afrika kuhusu utumishi wa umma limeanza Tanzania

20 Juni 2011

 

Kongamano la siku tatu la Umoja wa Mataifa na Afrika linalohusu utumishi wa Umma limeanza leo jijini Dar es Salaam ambako wajumbe zaidi ya 300 kutoka mataifa 80 wanajadilia mbinu mbalimbali za kuboresha utumishi wa umma.

Kongamano hilo ambalo ninafanyika kwa mara ya kwanza barani afrika na nchini Tanzania limeweka shabaya ya kujadili kwa kina ni kwa kiasi gani utumishi wa umma unavyoweza kuharakisha kuleta maendeleo kwa wananchi.

Utumishi wa umma unachukua nafasi kubwa kwenye harakati za ustawi wa jamii na barani Afrika inatajwa kwamba utumushi wa umma unatoa sehemu kubwa ya ajira inayofikia zaidi ya asilimia 70. 

George Njogopa amefuatialia kuanza kwa kongamano hilo na hii hapa taarifa yake.

(PKG NA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud