UM waainisha jukumu la wakunga katika kuokoa afya ya mama na mtoto

20 Juni 2011

Umoja wa Msataifa unazindua ripoti inayoainisha jukumu muhimu linalobebwa a wakunga ili kuhakikisha mamilioni ya wanawake na watoto wachanga hawapotezi maisha kirahisi wakati nchi nyingi bado zinapungukiwa na wataalamu wanaohitajika kuwasaidia kia mama wakati wa kujifungua.

Ripoti hiyo ‘Hali ya ukunga duniani 2011, kujifungua salama,kuokoa maisha” ni ya kwanza ya aina yake na inajumuisha takwimu zilizokusanywa katika nchi 58 duniani.

Ripoto hiyo ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa likiwemo la idadi ya watu duniani UNFPA, la watoto UNICEF, la afya duniani WHO na wadau zaidi ya 20 wa kimataifa itatolewa rasmi Jumatu ya leo June 20 kwenye mkutano wa kimataifa wa wakunga njini Durban Afrika ya Kusini.

Ripoto inathamini hatua zilizopigwa hadi sasa katika kuongeza idadi ya wakunga ambao ni muhimu hasa katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia mawili, kwanza kuboresha afya ya mama na kupunguza vifo vya watoto wakati wa kujifungua.

(SAUTI YA VICENT FAVEAU)

Dunia bado iko nyuma katika kufikia malengo hayo na mwaka jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alizindua mkakati maalumu kwa ajili ya afya ya wanawake na watoto kujaribu kuchapusha hatua katika masuala hayo.

Mkurugenzi mkuu wa UNFPA Babatunde Osotimehin ambaye ataziindua rasmi ripoti hiyo amekadiria kwamba takriban wanawake 900 wanakufa kila siku na wengine zaidi ya 34,000 wanakabiliwa na matatizo wakati wa kujifungua.

Katika baadhi ya nchi masikini kabisa duniani asilimia ndogo ambayo ni 13 ya wanawake wanaojifungua ndio wanaosaidiwa na wakunga au wataalamu wenye ujuzi unaohitajika. Wakunga takriban 3,000 wanaoshiriki mkutano wa Durban wanatarajiwa kuandamana mjini kana ishara ya nia yao ya kuboresha viwango vya huduma ya uzazi duniani.