Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliowauwa walinda amani wa MONUSCO wahukumuwa DR Congo

Waliowauwa walinda amani wa MONUSCO wahukumuwa DR Congo

Watu  wanne miongoni mwa tisa wanaodaiwa kuwa waasi waliowawa askari watatu walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO miezi tisa iliyopita wamekatiwa hukumu na mahakama ya kijeshi nchini humo.

Watu hao wamesomewa hukumu yao mjini Goma Kivu ya Kaskazini Mashariki mwa Congo, wilaya ambayo walitekeleza mauaji hayo baada ya kuvamia ofisi za Umoja wa Mataifa.  Na hukumu hizo ni kuanzia kifungo cha kifo, kwenda jela maisha na wengine miaka kadhaa.

Mbali ya kufanya mauaji washitakiwa hao wanadaiwa kupora silaha na fedha taslimu dola za kimerekani 1000. Mwandishi wa kujitegemea Mashariki mwa Congo Mseke Dide amefuatilia hukumu hiyo na kutuandalia taarifa hii.

(RIPOTI YA MSEKE DIDE)