Baraza la haki za binadamu lapitishwa mwongozo mpya kwa makampuni ya biashara

17 Juni 2011

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeridhia kwa kauli moja misingi mipya ya kimataifa ambayo inataka makampuni ya kibiashara duniani kote yanaendesha shughuli zake kwa kuheshimu haki za binadamu.

Mwongozo huo mpya unaainisha ni kwa kiasi gani nchi pamoja na wafanyabiashara zinawajibika kutekeleza kwa vitendo matamko ambayo yanasema kuwa “ kulinda, kuheshimu na utayari” juu ya haki za binadamu.

Kwa mujibu wa mwongozo huo wahusika wote wanapaswa kuhakikisha mwenendo wa uendeshwaji wa biashara zao hauvuki mipaka ya uvunjifu wa haki za binamu na umesisitiza kuwa utekelezaji wake umesimamia kwenye maeneo matatu.

Akielezea hatua hiyo Katibu Mkuu wa baraza hilo la haki za binadamu John Ruggie amesema kuwa kuanzishwa kwa mwongozo huo ni hatua muhimu katika uso wa dunia ambayo inajaribu kuweka mahusiano ya karibu baina ya biashara na haki za binadamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter