IOM yatiliana saini na Ecuador ili kukabili ongezeko la biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu

17 Juni 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limetiliana saini ya makubalino na mamlaka ya Ecuador ikiwa ni hatua yake ya kukabiliana na wimbi la usafirishaji haramu wa binadamu.

Makubaliano hayo ambayo yamesainiwa wiki hii yanatazamiwa kusaidia juhudi za kukabili biashara hiyo hasa katika eneo lililoko kusini ambako kunakutikana miji ya Lago Agrio na San Lorenzo. Taarifa zisizo rasmi na ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko kubwa la usafirishaji haramu wa binadamu ambao hutumikishwa kwenye madanguro ya ngono na pamoja na kazi nyingine za kinyonyaji.

Afisa wa IOM Rogelio Bernal, amesema kuwa kupitia makubaliano hayo kunatazamiwa kuimarishwa uwezo wa kiutendaji pamoja na mbinu za kisasa zitakazosaidia kukabiliana na biashara hiyo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter