Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washinikizwa kuajiriwa wanawake zaidi kwenye polisi wake

UM washinikizwa kuajiriwa wanawake zaidi kwenye polisi wake

Wanawake zaidi wanaajiriwa ili kutimiza asilimia 20 ya wanawake wanaohudumu kwenye polisi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani ifikapo mwaka 2014.

Mshauri wa polisi kwenye Umoja wa Mataifa Anne-Marie Orler anasema kuwa kati ya zaidi ya polisi 14,000 wanaohudumu sehemu mbali mbali zaidi ya 1,400 kati yao ni wanawake. Anasema kuwa idadi kubwa ya nchi zinaunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa za kuongeza idadi ya polisi wanawake wanaohudumu kwenye oparesheni za kulinda amani.

Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa mpango huo polisi waliajiriwa kwa ujumla ni 3000 huku idadi ya wanawake ikiongezeka kutoka asilimia 7.9 hadi asilimia 10.