Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano unaojadili uhamiaji uliochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa waandaliwa Bangkok

Mkutano unaojadili uhamiaji uliochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa waandaliwa Bangkok

Wataalamu kutoka Asia , Pacific , Marekani na Ulaya wanakutana mjini Bangkok hii leo kujadili athari za mabadailiko ya hali ya hewa. Mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na benki ya maendeleo barani Asia na shirika la kimataifa la uhamoaji IOM unajiri baada ya mkutano wa kwanza ulioandaliwa mjini Geneva tarehe 9 mwezi Juni ili kuweka sera na ufadhili katika kukabilizna na na uhamiaji uliochangiwa na madadiliko ya hali ya hewa.

Wanaohudhuria mkutano huo wakiwemo watunza sera na wasomi wanajadili matokeo ya mwisho ya mradi huo yaliyoorodheshwa kwenye ripoti iliyochapishwa mwezi Februari. Asia na Pacific ni kati ya maeneo yanayotarajiwa kuathirika na mabadiliko ya hali ya hewa na uhamiaji unaochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa.