Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahitimisha ziara nchini Brazil

Ban ahitimisha ziara nchini Brazil

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amehitimisha ziara yake nchini Braliz ambako katika mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Rousseff amemweleza kwamba kuanzia Septemba mwaka huu Rais huyo atakuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Umoja wa mataifa kufungua mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Ban ameishukuru Brazil kwa juhudi zake za kuchagiza maingiliano ya kikanda na uushirikiano wa Kusini-Kusini na pia kuwa kinara katika suala la upokonyaji silaha.

Viongozi hao wawili pia wamejadili mkutano ujao wa mabadiliko ya hali ya hewa Rio+20, mabadiliko kwenye baraza la salama la Umoja wa Mataifa na jukumu muhimu la Brazili kwenye ulinzi wa amani hasa Haiti.

Na katika mkutano na waandishi wa habari uliomshirikisha waziri wa mambo ya nje wa Brazili Antonio Patriota Ban ameipongeza Brazili kwa kupanua wigo wa jukumu lake kikanda na kimataifa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)