Mahakama ya ICC imewataka waathirika na walioshuhudia uhalifu Ivory Coast kutoa ushaidi

17 Juni 2011

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC Luis Moreno Ocampo ametoa mwaliko kwa waathirika wa madai ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotekelezwa nchini Ivory Coast na uapande wowote baada ya uchaguzi wa 2010 kujitayarisha kutoa shahidi wakati ICC inajiandaa kwa uchunguzi wa madai hayo.

Mwendesha mashitaka huyo amewaarifu waathirika wa machafuko kwamba wanaweza kutuma maoni yao kwa jaji wa mahakama hiyo endapo uchunguzi dhidi ya madai hayo ya uhalifu uanzishwe ama la. Waathirika hao au mawakili wao wana siku 30 kuanzia siku ya taarifa hii kuwasilisha maoni yao kwenye mahakama ya ICC imesema taarifa maalumu ilioyotolewa na ofisi ya mwendesha mashitaka huyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter