Hali ya usalama kwenye jimbo la Kordofan bado ni tete:OCHA

17 Juni 2011

Hali ya usalama kwenye jimbo la Kusini la Kordofan nchini Sudan bado ni mbaya limesema shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa mataifa OCHA.

Umoja wa Mataifa na OCHA wametoa wito kwa pande zote husika kwenye machafuko hayo kuruhusu misaada ya kibinadamu kuweza kuingizwa kwa maelfu ya wakimbizi wa ndani na waliosambaratishwa na machafuko hayo, pia kuruhusu walioatawanywa na mapigano kupita bila bughudha kwenda kwenye maeneo yenye usalama.

Kwa mujibu wa OCHA usalama mdogo na mapigano yanayoendelea yanakuwa kikwazo kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu kuwafikiwa maelfu ya wanaohitaji msaada. Shirika hilo limesisitiza haja ya kuwepo fursa ya kuwafikia watu hasa mji mkuu Kadugli na El Obeid. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter