Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauwaji ya mandishi wa habari India ya laaniwa vikali

Mauwaji ya mandishi wa habari India ya laaniwa vikali

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na utetezi wa uhuru wa vyombo vya habari ameshutumu na kulaani vikali tukio la mauwaji ya mwandishi wa habari mmoja wa India ambaye mauwaji yake yanasadikika kufungamanishwa na hatua zake za kuripoti juu ya mwenendo wa biashara ya mafuta kwa njia ya Mafia inayofanywa magharibi wa mji wa Mumbai.

Mkuu huyu Irina Bokova ameitolea mwito mamlaka za dola kuchunguza mauaji ya mwandishi Jyotirmoy Dey ambaye aliuwawa hapo  June 11.Amesema inasikitisha na kuvunja moyo kuona waandishi wa habari wanaotimiza wajibu wao lakini wanakumbwa na matukio kama hayo ambayo yanakwenda kinyume na misingi ya uhuru wa kutoa na kupata habari.

Bwana Dey alikuwa mwandishi wa habari mwandamizi na aliyebobea kwenye masuala ya habari za uchunguzi katika gazeti la kila siku la Midday. Katika siku za hivi karibuni alikiuwa akifuatilia mwenendo wa biashara ya kimafia ya mafuta.