Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yazitaka serikali za kiafrika kuwalinda watoto kutokana na dhuluma na unyanyasaji

UNICEF yazitaka serikali za kiafrika kuwalinda watoto kutokana na dhuluma na unyanyasaji

Ripoti ya shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF iliyotolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kiafrika yenye kauli mbiu “sote pamoja kwa hatua za haraka kuwapendelea watoto wa mitaani” inasema kuwa maelfu ya watoto barani Afrika wanapitia dhuluma na unyanyasaji kila siku hasa wale wanaoishi na kufanya kazi kwenye mitaa.

UNICEF inatoa wito kwa serikali kuwa na mipango ya kuwahakikishia mazingira salama familia na jamii ili kuwalinda watoto na pia kuwahakikishia huduma zikiwemo za kiafya na za elimu.

George Njogopa na taarifa kamili