Washindi wa tuzo la idadi ya watu la UM kutuzwa hii leo

16 Juni 2011

 

Tuzo la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa litatolewa hii leo kwenye sherehe zitakazoandaliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Kila mwaka kamati ya Umoja wa Mataifa ya tuzo la idadi ya watu inamtunuku mtu au watu au taasisi kwa kuchangia katika kutoa hamasisho kuhusu maswali ya idadi ya watu na suluhu zake.

Washindi wa tuzo la mwaka huu ni Professor Mohammad Jalal Abbasi-Shavazi kutoka Iran na taasisi inayotoa mafunzo kuhusu masuala ya idadi ya watu kutoka nchini Cameroon. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ndiye atatoa tuzo hizo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter