Kunamengi ya kufanywa ili kuimarisha shughuli za utoaji misaada ya usamaria wema-UM

16 Juni 2011

Kumekuwa na changamoto kubwa za kiusalama zinazowakabili wafanyakazi wa misaada ya kiutu na waangalizi wa amani pindi wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kuwajali wale wenye mahitajio.

Kulingana na Naibu Mkuu wa kitengo cha umoja wa mataifa kinachohusika na misaada ya usamaria mwema OCHA Bi Catherine Bragg  kuna haja sasa ya kupitia upya taratibu na mikakati ili kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinafifishwa kwa maslahi ya wote. Ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo kutatoa fursa nzuri ambayo itasaidia pakubwa kuimarisha shughuli za usamaria mwema duniani kote.

Katika harakati za uimarishwaji wa shughuli hizo, mapema mwezi huu Bi Catherine alitembelea Jamhuri ya Congo ambako kumekuwa na kiwango kikubwa cha matukio ya unyanyasaji ulioenda sambamba na kushamiri kwa vitendo vya kihalifu. Watu zaidi ya milioni 1 wameingia kwenye maisha ya ukimbizi kulikosababishwa na machafuko ya muda mrefu katika taifa hilo la DRC.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter