Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa kitendo cha mambo ya siasa UM afanya mazungumzo na viongozi wa Iraq

Mkuu wa kitendo cha mambo ya siasa UM afanya mazungumzo na viongozi wa Iraq

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya siasa amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Iraq kwa kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali juu ya ustawi wa taifa hilo.

Lynn Pascoe alizuru mjii mkuu Bagdad na baadaye kutembelea miji mingine ya Kirkuk na Erbil ambako pia alikutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa walioko nchini humo. Akizungumza wakati wa ziara yake hiyo, kiongozi huyo alisisitiza juu ya utayari wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuipiga jeki Iraq ambayo ipo kwenye mpito wa ujenzi mpya wa demokrasia. 

Aidha amewapongeza wananchi wa Iraq pamoja na wafanyakazi wa kimataifa ambao amesema kuwa wamefanya kazi kubwa pamoja na kukabiliwa na kipindi kigumu.