Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa Afrika wasema una nia ya kutatua mzozo wa Libya

Muungano wa Afrika wasema una nia ya kutatua mzozo wa Libya

Mchakato wa kutatua mzozo wa Libya lazima ujumuishe maafikiano ya pande zote na mazungumzo yasiyo na masharti umesema muungano wa Afrika hii leo, ukiuhakikishia Umoja wa Mataifa nia yake ya kujiunga na juhudi za kutafuta suluhisho la machafuko ya Libya litakalojumuisha pande zote.

Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama kwa niaba ya muungano wa Afrika hii leo waziri wa mambo ya nje wa Mauritania Hamady Ould Hamady amesema wamekuja kusema kwamba ni muhimu mchakato huo wa suluhu uendeshwe na kumilikiwa na watu wa Libya, ukijumisha muafaka kwa njia ya majadiliano bila masharti.

Amesisitiza haja ya mchango wa Afrika katika juhudi za kupata suluhisho na ushirikiano wa karibu kati ya makundi yote yaliyo na dhamira ya kutatua mzozo wa Libya.

Ameongeza kuwa muungano wa Afrika utasalia kuwa mwaminifu na mshirika wa Umoja wa Mataifa kwa ujumla na hasa kwa baraza la usalama na tajitahidi kwa kila hali kuwasaidia watu wa Libya katika mazingira yoyote yale.

Ameongeza kuwa mpango wa muungano wa Afrika katika kutatua machafuko ya Libya ni pamoja na wito wa kusitisha mara moja mapigano, kutaka ushirikiano wa serikali ya Libya katika kusaidia kufikisha misaada ya kibinadamu, kuwalinda raia wa kigeni ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wahamiaji na kufanya mabadiliko ya kisiasa ambayo yatakata mizizi ya. chanzo cha machafuko